Thursday, May 16, 2013

MICHUANO YA WTA ITALIAN OPEN YAIVA JIJINI ROME.

MWANADADA nyota wa tenisi anayeshika namba mbili katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake, Maria Sharapova ameanza vyema michuano ya wazi ya Italia kwa kumfunga Garbine Muguruza wa Hispania. Sharapova raia wa Urusi ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo alifanikiwa kumgaragaza Muguruza kwa 6-2 6-2 katika mchezo uliofanyika jijini Rome jana. Akizungumzia mchezo huo mwanadada huyo mwenye mvuto amesema mashindano hayo yana maana kubwa kwake kwasababu ameanza kucheza hapo toka akiwa binti mdogo. Kwa upande mwingine Victoria Azarenka anayeshika namba tatu kwa ubora alifanikiwa kumfunga kirahisi Julia Goerges wa ujerumani kwa 6-2 6-0 na Li Na naye alifanikiwa kumchapa raia mwenzake wa China Zheng Jie kwa 6-3 6-1.

No comments:

Post a Comment