Thursday, May 16, 2013

MARA NYINGINE NITATOKA UWANJANI KAMA MASHABIKI WABAGUZI WAKIENDELEA KUNINYANYAPAA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Italia na klabu ya AC Milan ya Italia, Mario Balotelli amesema ataondoka uwanjani mara nyingine mashabiki watakapomnyanyapaa kwa rangi yake. Katika mahojiano aliyofanya na kituo cha luninga cha CNN Balotelli amesema ilibaki kidogo aondoke uwanjani baada ya kutukanwa na mashabiki wa klabu ya AS Roma katika Uwanja wa San Siro Jumapili iliyopita. Nyota huyo amesema kama tukio kama hilo litajitokeza tena hatasita kutoka uwanjani kwasababu ni jambo la kipuuzi linalofanywa na mashabiki wabaguzi. Alipoulizwa kitu kilichomzuia kutoka uwanjani kwenye mechi hiyo Balotelli alidai kutokana na mchezo wenyewe ulivyokuwa alifikiri kama angetoka watu wangedai ameondoka kwasababu mchezo umekuwa mgumu. Kutokana na tukio hilo ambalo lilisababisha mchezo kusimamishwa kwa dakika kadhaa ili kuwatuliza mashabiki hao Roma walipigwa faini ya euro 50,000 na kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Italia.

No comments:

Post a Comment