Thursday, May 16, 2013
PELE ATAKA UWANJA WA MARACANA UMILIKI UACHWE KWA WANANCHI WA BRAZIL.
NGULI wa soka wa Brazil, Pele jana amepingana vikali katika mjadala kuhusu mustakabali wa Uwanja wa Maracana akidai kuwa uwanja huo haupaswi kubinafsishwa kama baadhi ya maofisa wanavyotaka baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota huyo wa zamani amesema uwanja huyo unamilikiwa na watu akimaanisha wananchi wa Brazil hivyo hakubaliani na wazo la kuubinafsisha. Kauli ya Pele imekuja wakati akizindua mpango wa kutengeneza filamu kuhusu maisha yake ambaye imepangwa kutoka kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Dunia 2014. Pele ambaye anahesabika kama mmoja wa wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka, aliibuka kutoka katika lindi la umasikini na kuwa shujaa kwa kuisaidia nchi hiyo kunyakuwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1958. Uwanja wa Maracana ambao ulijengwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1950 kwasasa unaendelea na matengenezo ya kuuboresha kwa gharama ya dola milioni 430 zilizotolewa na serikali ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment