
Tuesday, May 7, 2013
PEPE ANA MATATIZO - MOURINHO.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho amemjibu Pepe kufuatia kauli ya beki huyo aliyoitoa hivi karibuni kuhusu mahusiano ya Mouringo na golikipa Iker Casillas. Pepe alikaririwa akisema kuwa kocha huyo inapaswa amuheshimu zaidi Casillas baada ya mchezo wa mwishoni mwa wiki ambao Madrid walishinda kwa mabao 4-3, lakini Mourinho amesema kuwa mchezaji huyo amezua mjadala huo kwasababu yeye mwenyewe anapigania namba katika kikosi cha kwanza. Mourinho amesema ni kazi rahisi kuchambua alichosema na amegundua kwamba Pepe ana matatizo na tatizo lake kubwa ni Raphael Varane ambao wanagombea namba katika kikosi cha kwanza. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa Pepe amenyang’anywa namba na kijana huyo mwenye miaka 19 ndio maana anatafuta pa kulaumu wakati jambo la msingi ni kuongeza bidii ili aweze kurejea katika nafasi yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment