Tuesday, May 7, 2013

MJUMBE MWINGINE WA FIFA ASIMAMISHWA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeendelea kujisafisha taratibu baada ya mjumbe wake wa kamati ya utendaji Chuck Blazer kusimamishwa jana ikiwa ni chini ya mwezi mmoja baada ya kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha akiwa kama katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la nchi za Amerika Kaskazini, Kusini na Carribean-CONCACAF. Blazer mwenye umri wa miaka 68 raia wa Marekani ambaye ilikuwa aachie nafasi hiyo ya kamati ya utendaji Mei 30 amesimamishwa na kamati ya maadili ya FIFA. Shirikisho hilo limedai kuwa wamefikia uamuzi huo kwasababu Blazer ameonekana kukiuka sheria mbalimbali za maadili za FIFA. Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya mjumbe mwingine wa kamati ya utendaji wa FIFA Vernon Manilal Fernando wa Sri Lanka kufungiwa miaka nane kwa kosa la ukiukwaji wa maadili.

No comments:

Post a Comment