
Tuesday, May 7, 2013
HOENESS KUENDELEA NA WADHIFA WAKE.
BODI ya usimamizi wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, imemuwashia taa ya kijani Uli Hoeness kuendelea na wadhifa wake wa urais wa klabu hiyo baada ya ombi lake la kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa ukwepaji kodi kukataliwa na bodi hiyo. Pamoja na Hoeness mwenye umri wa miaka 61 kukamatwa mwezi uliopita na baadae kuachiwa kwa dhamana ya euro milioni tano kama sehemu ya kuendelea kwa uchunguzi dhidi yake ya ukwepaji kodi katika moja ya akaunti yenye jina lake iliyopo Switzerland, bodi hiyo bado imeonyesha kuwa na imani naye. Bayern wana kibarua kizito cha kuhakikisha inakuwa timu ya kwanza nchini Ujerumani kunyakuwa mataji matatu makubwa ambayo ni Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga, Kombe la Ligi na lile la Champions League ambalo wataenda kulitafuta Wembley Mei 25. Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel aliwahi kunukuliwa kusikitishwa na kashfa inayomkabili Hoeness ambaye ni mfano wa kuigwa nchini humo. Hoeness mara mbili ameshanusurika kufa, mara ya kwanza ikiwa ni katika ajali ya gari mwaka 1975 na baadae mwaka 1982 katika ajali ya ndege ambayo iliwaua marafiki zake watatu aliokuwa nao wakati alikutwa baadae akitembea karibu na eneo hilo huku akiwa katika mshtuko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment