Tuesday, May 7, 2013

RIISE ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA.

BEKI wa kimataifa wa Norway, John Arne Riise ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa baada ya kuitumikia timu yake ya taifa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 13. Riise anayekipiga katika klabu ya Fulham ya Uingereza ambaye alianza kuitumikia nchi yake Januari mwaka 2000 katika mechi dhidi ya Iceland amecheza mechi 110 na kufunga mabao 16 katika kipindi chote hicho.Mchezaji huyo ndiye aliyeichezea nchi yake mechi nyingi zaidi kwa kipindi chote lakini ameamua kutundika daluga ili aweze kuhamishia nguvu zake katika klabu yake. Riise amesema amefikia uamuzi huo baada ya kufiri sana na kuona kwamba anaelekea katika kipindi cha mwishoni cha uchezaji soka hivyo amemua kuhamishia nguvu zake klabuni ili aweze kucheza kwa muda mrefu zaidi.

No comments:

Post a Comment