
Tuesday, May 7, 2013
FIFA KUONGEZA WAAMUZI.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetoa mapendekezo ya kuongeza waamuzi viwanjani ili kuangalia matukio ya kibaguzi na kuongeza mifumo miwili ya adhabu kwa timu ambazo mashabiki wake wana tabia hizo za kibaguzi. Katika taarifa FIFA imesema kuwa waamuzi wapya watakaoongezwa kazi yao kubwa itakuwa kufuatilia matukio ya kibaguzi ili kupunguza msukumo kwa mwamuzi wa kati na pia watakuwa wakikusanya ushahidi kusaidia kamati ya nidhamu. Kwenye mkutano huo wa FIFA wa kupambana na ubaguzi wa rangi pia walipendekeza kuwa makosa madogo ya kwanza adhabu zake ziwe kucheza katika vianja vitupu, onyo au faini huku makosa makubwa au waakaorudia makosa watapewa adhabu ya kukatwa alama, kuenguliwa katika mashindano husika au kushushwa daraja. Mapendekezo hayo yote yanatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa FIFA utakaofanyika nchini Mauritius mwishoni mwa mwezi huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment