
Monday, May 6, 2013
DORTMUND YAPOKEA MAOMBI NUSU MILIONI YA TIKETI ZA FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE.
KLABU ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imedai kupokea maombi zaidi ya nusu milioni ya tiketi kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya wajerumani wenzao Bayern Munich. Borussia ambao wana wastani wa kupata mashabiki 80,000 katika uwanja wao wa nyumbani wamesema mashabiki 502,567 wameomba tiketi kwa njia ya mtandao kabla ya muda wa mwisho ambao ulikuwa Jumapili. Klabu hiyo imesema imeshangazwa kupata idadi hiyo kubwa ambapo sasa itabidi wafanye droo ili mashabiki hao waweze kupata tiketi 24,042 walizopewa kwa mchezo huo utakaochezwa Mei 25 mwaka huu. Timu mbili zilizotinga fainali ya michuano hiyo zimepewa jumla ya tiketi 50,000 za Uwanja wa Wembley ingawa uwanja huo una uwezo wa kubeba mashabiki 86,000. Bei ya tiketi hizo inaanzia paundi 60 kwa tiketi mpaka paundi 330 bei ambazo ni ngeni kwa mashabiki wa Ujerumani ambao wamezoea kupata tiketi za bei ya chini katika mechi za Bundesliga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment