Monday, May 6, 2013

BAFANA BAFANA, CAR KUCHEZA JIJINI YAOUNDE.

TIMU ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana inatarajia kucheza mchezo wake wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR katika uwanja huru jijini Yaounde, Cameroon June 9 mwaka huu. Hatua hiyo imekuja kufuatia Chama cha Soka nchini Afrika Kusini-Safa ambao waliomba Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na lile la Afrika-CAF kubadilishiwa uwanja katika mchezo wao wa marudiano kutokana na vurugu za kisiasa huko CAR. Wanajeshi wapatao 13 wa Afrika Kusini walifariki kufuatia mapigano katika mji mkuu wan chi hiyo Bangui miezi iliyopita huku idadi hiyo ikiongezeka na kufikia 14 baada ya mwanajeshi mmoja aliyejeruhiwa naye kufariki mwezi uliopita. Kocha wa Bafana Bafana aliusifu uamuzi huo wa FIFA na CAF kubadilisha uwanja haswa kutokana na tukio la kuuwawa kwa wapendwa wao katika kipindi kifupi kwenye eneo hilo.

No comments:

Post a Comment