RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amesema anataka polisi wa michezo barani humo kupambana na mambo ya kamari, rushwa, upangaji matokeo na wahuni katika soka. Katika taarifa yake aliyoitoa kwenye hotuba yake jijini London, Paltini amesema miaka sita toka alipopendekeza kuwepo kwa vikosi vya usalama katika michezo hajaona mabadiliko yoyote kutoka kwa serikali za nchi barani humo. Platini amesema atawaomba wajumbe kutoka nchi 53 wa UEFA kuweka sheria rasmi ya suala la upangaji wa matokeo ili wahusika waweze kupata adhabu stahiki kwa kutemnda kosa hilo. Platini ambaye ni mchezaji nyota wa zamani wa Ufaransa amesema katika mapendekezo yake hayo ni nchi 10 pekee ndio zilizotengeneza sheria hizo.
No comments:
Post a Comment