Saturday, May 25, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINAL: NANI KUTOKA ANACHEKA WEMBLEY?

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inafikia kilele leo kwa mchezo wa fainali utakaozikutanisha timu za Ujerumani Bayern Munich na Borussia Dortmund mtanange ambao utafanyika katika Uwanja wa Wembley jijini London, Uingereza. Hiyo ni fainali ya kwanza kabisa kuwahi kuzileta pamoja timu mbili za Bundesliga katika historia ya michuano hiyo mikubwa kabisa ya vilabu barani humo. Safari ya timu hizo kufikia fainali haikuwa rahisi kwani Bayern walilazimika kuwafunga Barcelona kwa jumla ya mabao 7-0 katika mechi za mikondo miwili walikutana katika hatua ya fainali huku Dortmund wao wakiizamisha Real Madrid kwa jumla ya mabao 4-1 matokeo yaliyowashangaza wadau wa soka duniani kote. Bila kujali matokeo ya mechi ya leo, bila shaka utakuwa usiku wa kihistoria kwa soka la Ujerumani, lakini timu hizo mbili zinashuka dimbani zikiwa na motisha tofauti. Kwa Bayern, hiyo ni fursa ya kujikomboa kutokana na machungu waliyopata katika vichapo vya fainali za mwaka wa 2010 na hasa mwaka wa 2012 wakati walipofungwa na Chelsea kwa changamoto ya mikwaju ya penati, fainali ambayo ilichezwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.

No comments:

Post a Comment