
Sunday, May 5, 2013
RONALDO AWANYIMA RAHA BARCELONA.
VINARA Barcelona watalazimika kusubiri kwa wiki nyingine kushangilia taji la La Liga baada ya Cristiano Ronaldo kufunga mabao mawili katika ushindi wa Real Madrid inayoshika nafasi ya pili wa mabao 4-3 wakitokea nyuma dhidi ya Real Valladolid jana. Kama Madrid isingeshinda, ushindi wa Barca dhidi ya Real Betis katika Uwanja wa Nou Camp baadae leo ungewahakikishia taji la nne ndani ya miaka mitano, wakiwa kileleni kwa pointi 13 zaidi zikiwa zimebaki mechi nne zenye wastani wa pointi 12. Valladolid, ambayo haijachukua pointi Bernabeu kwa zaidi ya muongo, ilipata bao la kuongoza dakika ya nane wakati Oscar Gonzalez alipomtungua kipa wa Madrid, Diego Lopez. Real ilisawazisha dakika ya 26 wakati Marc Valiente alipobabatiza shuti la Angel Di Maria na kujifunga, kabla ya Ronaldo kufunga bao lake la kwanza jana kwa kichwa dakika sita baadaye. Valladolid ilifunga bao lake la tatu kupitia kwa Javi Guerra dakika ya 35 na Kaka akaisawazishia tena Real dakika nne baadaye kabla ya roaldo kufunga bao la ushindi dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment