
Sunday, May 5, 2013
WENGER ATAMBA ARSENAL KUMALIZA KATIKA TOP FOUR.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ametamba kuwa kikosi chake kina kasi ya kutosha kuhakikisha kinapambana na kupata nafasi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kikosi cha Wenger kimejongea tena katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kuifunga Queens Park Rangers ambayo imeshuka daraja kwa bao 1-0 na kuweka pengo la alama mbili mbele ya Chelsea ambao wana kibarua kigumu dhidi ya Manchester United. Wakiwa hawajafungwa katika mechi nane walizocheza, na sasa wana mechi mbili zilizosalia Wenger anaamini kwa kasi waliyonayo kuna uhakika wa kutosha wa kumaliza katika nafasi nne za juu. Wenger amesema kwasasa hafikirii kuangalia timu ambazo zinagombea nafasi hiyo matokeo watakayopata kitu cha msingi ni kuhakikisha wanashinda mechi zao zilizosalia na kumaliza wakiwa na alama za juu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment