Sunday, May 5, 2013

MAYWEATHER, KLITSCHKO WASHINDA MAPAMBANO YAO.

BONDIA Floyd Mayweather Jnr ametoka gerezani na kuendeleza ubabe katika ndondi kwa kushinda pambano la uzito wa Welter dhidi ya Robert Guierrero kwa alama. Robert Guerrero alishindwa pointi 117-111 zilizotolewa na majaji wote waliompa ushindi Mayweather. Wengi walikuwa wana wasiwasi baada ya Mayweather kutoka jela angeathirika kimchezo, lakini usiku wa jana alikuwa moto mkali. 
Kwa upande mwingine bondia bingwa wa uzito wa juu dunia Wladimir Klitschko amefanikiwa kutetea mataji yake kwa kumpiga bondia ambaye hajawahi kupigwa Francesco Pianeta kwa knockout kwenye mzungumzo wa sita. Ulikuwa ni ushindi wa 51 wa knockout kwa bondia huyo raia wa Ukraine anayeshikilia mataji ya WBA, WBO, IBF na IBO huku akiendeleza rekodi yake ya kucheza mapambano 60 na kupigwa matatu pekee. Pambano hilo lilikuwa somo kwa bondia David Haye ambapo alikuwa jukwaani akishuhudia kabla ya pambano lake na Manuel Charr litakalofanyika jijini Manchester Juni 29 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment