
Sunday, May 5, 2013
SINA MPANGO WA KUIACHA UNITED - FERGUSON.
MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema hana mpango wa kuachia wadhifa wake huo baada ya klabu hiyo kuthibitisha kwamba atafanyiwa upasuaji katika kipindi cha majira ya kiangazi. Ferguson mwenye umri wa miaka 71 atafanyiwa upasuaji wa nyonga lakini amesisitiza kuwa mipango yake aliyonayo haitaathirika. Kocha huyo amesema siku zote ni vigumu katika soka kuwa na uhakika na kitakachotokea mbele lakini pamoja na hayo hana mpango wa kuondoka katika kitu ambacho anaamini kitakuwa cha kipekee na cha thamani kuwa karibu kukitizama. Ferguson ameiongoza Manchester United kushinda taji la 13 la ligi na anategemea kuongeza taji lingine msimu ujao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment