 |
Johan Cruyff enzi zake. |
MCHEZAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Barcelona Johan Cruyff ameponda madai kuwa zamani za ushindi za klabu hiyo zimeelekea mwishoni. Pamoja na kung’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kukubali kichapo cha mabao 7-0 katika mechi mbili walizokutana na Bayern Munich ya Ujerumani, kikosi cha timu hiyo ambacho kinanolewa na Tito Vilanova bado kiko katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la 22 la La Liga.
 |
Johan Cruyff alivyo sasa. |
Ambapo Cruyff amesema mafanikio iliyopata timu hiyo katika ligi ambayo aliwahi kuiwakilisha akiwa kama mchezaji na baadae kocha ni ushahidi tosha kuonyesha kwamba timu hiyo ina uwezo wa kushindana kwa kiwango cha juu. Cruyff amesema ni suala la kipuuzi mtu kudai enzi za Barcelona zimekwisha kwani katika soka timu siku zote huwa inakwenda juu na kurudi chini cha msingi ni kuangalia changamoto zilizowakabili msimu huu ili msimu ujao wawe bora zaidi.
No comments:
Post a Comment