
Monday, May 6, 2013
VILANOVA KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA.
MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova anaweza kukosa sherehe kama timu hiyo itatangazwa bingwa mpya wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga Jumatano kwa sababu atakuwa jijini New York kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Ushindi wa mabao 4-2 waliopata dhidi ya Real Betis jana umeacha pengo la alama 11 mbele ya mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili huku wakibakiwa na mechi nne ambazo watahitaji alama mbili pekee ili waweze kufikisha alama ambazo hazitaweza kufikiwa na timu nyingine. Madrid wanatarajiwa kuwakaribisha Malaga Santiago Bernabeu Jumatano ambapo kama Madrid wakishindwa kushinda kwenye mchezo moja kwa moja Barcelona atatangazwa bingwa mpya likiwa ni taji lao nne ndani ya miaka mitano. Vilanova alitumia muda wa miezi miwili jijini New York mapema mwaka huu akipatiwa matibabu ya mionzi kwa ajili ya kansa ya koo na kurejea Hispania Machi kuendelea na kibarua chake cha kuinoa Barcelona.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment