Monday, May 6, 2013

HOENESS KUJIUZULU URAIS WA BAYERN KWA MUDA.

RAIS klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Uli Hoeness anajipanga kutangaza leo kwamba atajiuzulu kwa muda baada ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mpaka hapo uchunguzi wa suala lake la ukwepaji kodi litakapomalizika. Hoeness mwenye umri wa miaka 61 amekuwa akishinikizwa kujiuzulu baada ya taarifa kuwa alikamatwa Machi 20 mwaka huu na baadae kuachiwa kwa dhamana ya kiasi cha euro milioni tano kama sehemu ya uchunguzi wa ukwepaji kodi. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya Ujerumani, Hoeness anatarajiwa kutangaza uamuzi wake baadae leo katika kikao cha bodi ya maofisa wa klabu hiyo. Bayern ambayo imetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuing’oa Barcelona kwa jumla ya mabao 7-0 katika mechi za mikondo walizokutana wanatarajiwa kumenyana na wajerumani wenzao Borussia Dortmund katika Uwanja wa Wembley Mei 25 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment