
Monday, May 6, 2013
RIBERY KUONGEZA MKATABA MUNICH.
WINGA machachari wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich Franky Ribery amesema ana nia ya kuongeza mkataba wake ambao utamalizika 2015 akiwa tayari ameitumikia klabu hiyo kwa miaka sita mpaka sasa. Ribery mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Bayern Julai mwaka 2007 akitokea klabu ya Olympique Marseille na amefunga mabao 51, pasi zilizozaa mabao 74 katika mechi 154 alizochezea timu hiyo na kujizolea sifa nyingi kwa mashabiki. Nyota huyo ambaye timu yake inatarajia kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund Mei 25 mwaka huu amesema ana furaha kuwepo katika klabu hiyo na haoni sababu ya kushindwa kuongeza mkataba mwingine. Kauli ya Ribery imekwenda sambamba na kauli ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Matthias Sammer ambaye amesema anataka kumfunga nyota huyo kwa mkataba wa muda mrefu ambao unategemea kusainiwa karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment