
Monday, May 6, 2013
MILAN, FIORENTINA ZAGOMBEA NAFASI YA TATU SERIE A.
PAMOJA na klabu ya Juventus kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu nchini Italia, Serie A lakini bado kuna ushindani kwa mechi zilizobakia baina ya vilabu vya AC Milan na Fiorentina wakigombea nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Katika vita hiyo Milan ndio wako katika nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi ya tatu mwa msimamo wa Serie A wakitofautiana kwa alama nne na Fiorentina ambao wako nafasi nne huku kukiwa kumebaki mechi tatu kabla ligi haijamalizika. Mechi za Serie zitaendelea tena JUmatano ambapo Milan itaifuata Pescara ambayo tayari imeshuka daraja huku Fiorentina wao wakiwa na kibarua kigumu zaidi pale watakapowakaribisha Siena ambao wanapambana wasishuke daraja. Makamu wa rais wa Milan Adriano Galliani amesema mchezo dhidi Piscara hautakuwa rahisi pamoja na kwamba tayari wameshashuka daraja hivyo kuwataka wachezaji kuwa makini na kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment