Thursday, May 23, 2013
SANTOS YAKATAA OFA YA BARCELONA KWA MARA YA PILI.
MAKAMU wa rais wa klabu ya Santos ya Brazil, Odilio Rodrigues amedai kuwa wamekataa ofa ya klabu ya Barcelona ya Hispania kutaka kumsajili mshambuliaji wao nyota Neymar kwa mara ya pili. Katika siku za karibuni Barcelona ndiyo pekee wameonyesha nia ya kumhitaji mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil na kuripoti kuwa walitaka kuwapa Santos euro milioni 20 ili waweze kumiliki haki za mchezaji huyo kwa asilimia 55. Wakati mahasimu wao nao wakiongeza kasi ya kumfuatilia mshambuliaji huyo, Barcelona walitoa kiasi hicho ili waweze kumaliza suala hilo lakini Rodrigues amesisitiza kuwa hawana haraka ya kumuuza Neymar kwa kiasi kidogo kuliko wanachotaka. Rodrigues alithibitisha kuwa ni kweli walipata ofa ya Barcelona kwa mara ya pili lakini waliikataa kwasababu hawakufikia kiwango walichokuwa wakikihitaji. Neymar katika siku karibu ameweka wazi nia yake ya kubakia Santos mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, ingawa uhamisho wa kwenda barani Ulaya katika kipindi hiki cha usajili unaonekana kama unaweza kuwepo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment