Thursday, May 23, 2013
LOEW ATAMANI MICHUANO YA EURO INGEKUWA MWAKA HUU.
KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amedai kuwa angependa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi ambayo itazikutanisha timu za nchi hiyo kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund ichezwe mwaka uliopita. Miezi 12 iliyopita, Bayern walitoka uwanjani wakiwa wametota kwa kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika fainali ya michuano hiyo na kocha huyo amedai kuwa fainali hiyo iliwapunguza morali wachezaji wa timu hiyo aliyowaita kwenye kikosi cha timu ya taifa ambacho kilishiriki michuano ya Ulaya 2012. Low amesema ari waliokuwa nayo wachezaji wa timu zote mbili pamoja na soka la Ujerumani kwa ujumla katika fainali hiyo ya Jumamosi ingesaidia sana kwa timu ya taifa kama michuano ya Ulaya ingekuwepo tena mwaka huu. Low ameanza kuinoa Ujerumani toka mwaka 2006 na mkataba wake unaishia baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment