Thursday, June 13, 2013
BARAKAT ATUNDIKA DARUGA.
MCHEZAJI mkongwe wa klabu ya Al Ahly ya Misri, Mohammed Barakat ametangaza kutundika daruga ifikapo mwishoni mwa msimu huu akiwa na umri wa miaka 36. Barakat ametangaza uamuzi huo baada ya kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake jijini Cairo kwa miaka tisa. Maofisa klabu hiyo walifanya mazungumzo na mchezaji huyo kujaribu kumshawishi aongeze mkataba lakini mwenye alikataa na kudai kuwa anataka kupumzika. Mchezaji huyo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwashukuru wachezaji, familia na mashabiki wote ambao wamekuwa pamoja kwa kipindi chote cha uchezaji wake. Kocha wa Al Ahly Mohammed Yousef amesema amesikitishwa na uamuzi wa mchezaji huyo kwani bado ni mmoja wa bora kabisa katika timu hiyo na Ligi Kuu nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment