Thursday, June 13, 2013

MIAKA SITA JELA YAMKABILI MESSI AKIKUTWA NA HATIA.

MSIMAMIZI wa masuala ya kisheria na fedha wa mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi aitwaye Angel Juarez amesisitiza kua mchezaji huyo bado hajataarifiwa kuwa tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili zimekifishwa katika vyombo husika. Juarez aliongeza kuwa kama kesi hiyo ikifunguliwa wanasheria wa nyota huyo wako tayari kwa ajili ya kumtetea mteja wao kwenye kesi hiyo dhidi ya mamlaka ya mapato nchini Hispania. Mwendesha mashitaka Raguel Amando ndio nachunguza tuhuma za nyota huyo wa Argentina pamoja na baba yake kukwepa kulipa kodi kutokana na mauzo ya haki za picha zake ambazo zinaendeshwa nje ya nchi hiyo. Mara baada ya taarifa hizo kutoka Messi alionyesha kushangazwa na tuhuma hizo na kudai kuwa hawajawahi kufanya udanganyifu wowote. Kwa sheria za Hispania, Messi anaweza kukumbwa na adhabu ya kufungwa miaka sita jela kama akikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo.

No comments:

Post a Comment