Saturday, June 8, 2013

BESIKTAS YAMNYATIA RONALDINHO.

MAKAMU wa rais wa klabu ya Besiktas ya Uturuki, Ahmet Nur Cebi amebainisha kuwa klabu hiyo ina mpango wa kumsajili mchezaji nyota wa klabu ya Atletico Mineiro, Ronaldinho katika kipidi hiki cha usajili majira ya kiangazi. Vigogo hao wa soka wa Istanbul wamepania kuongeza ubunifu zaidi katika kikosi chao kwa ajili ya msimu wa 2013-2014 na wanaona nyota huyo wa zamani wa Barcelona atawasaidia katika hilo. Cebi amesema tayari wameshazungumza na mchezaji huyo na kutoa ofa yao hivyo wanasubiri majibu kutoka kwake kama atakubali. Ronaldinho mwenye umri wa miaka 33 aliondoka barani Ulaya na kuhamia klabu ya Flamengo Januari mwaka 2011 na baadae kuhamia Mineiro mwaka 2012 baada ya kushindwana suala la malipo. Mkataba wa sasa wa Ronaldinho na Mineiro unamalizika Desemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment