Saturday, June 8, 2013

NIKO FITI KWA AJILI YA WIMBLEDON - MURRAY.

MCHEZAJI tenisi nyota wa Uingereza, Andy Murray anaamini kuwa kuikosa michuano ya wazi ya Ufaransa kunaweza kumsaidia katika maandalizi yake ya michuano ya Wimbledon inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi wiki ijayo. Murray ambaye anashika namba mbili katika orodha za ubora duniani hakushiriki michuano ya Ufaransa kwasababu ya kusumbuliwa na maumivu ya mgongo lakini sasa hivi yuko fiti kwa ajili ya kuanza msimu wa viwanja vya majani. Nyota amesema viwanja vya majani vinachukua muda kuvizoea lakini amekuwa akifanya mazoezi kwenye viwanja hivyo kwa zaidi ya siku 10 au zaidi tofauti na kama angekuwa ameshiriki michuano ya wazi ya Ufaransa. Ni mategemeo yake maandalizi aliyofanya yanaweza kumfanya afanye vyema kwenye michuano hiyo ambayo inachezwa katika ardhi ya nyumbani.

No comments:

Post a Comment