Saturday, June 8, 2013

KILA LA KHERI TAIFA STARS.

TIMU ya taifa ya Tanzania -Taifa Stars inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia wakati watakapoikabili Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade hapa Marrakech, Morocco. Stars katika mchezo wa kwanza waliocheza ugenini walipoteza dhidi ya Ivory Coast mwaka jana, na kushinda mechi zingine mbili mfululizo walizocheza nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco. Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake imepania mechi hiyo, lengo likiwa ni kuona inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mechi hiyo itakayokuwa chini ya mwamuzi Daniel Frazier Bennett wa Afrika Kusini. Mechi inatarajiwa kuanza kuchezwa saa tatu za usiku kwa saa za nchini Morocco ambapo hapa kwetu Tanzania itakuwa ni muda wa saa tano za usiku, mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Taifa Stars.

No comments:

Post a Comment