Sunday, June 9, 2013

SERENA BADO ANA KIU NA MATAJI ZAIDI.


MWANADADA nyota wa mchezo wa tenisi anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams wa Marekani amedai anataka kuendelea kubakia kiwango cha juu siku zote ili aweze kushinda mataji zaidi. Kauli ya Williams ameoitoa baada ya kufanikiwa kushinda taji lake la pili la michuano ya wazi ya Ufaransa kwa kumfunga Maria Sharapova wa Urusi kwa 6-4 6-4. Hilo linakuwa taji lake la 52 kwa mwanadada huyo toka aliposhinda taji lake la kwanza katika michuano ya ndani ya Ufaransa mwaka 1999 na toka wakati huo amekuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa waliopata kutokea katika kipindi chote. Williams amesema kwasasa bado anataka kushinda mataji zaidi mpaka atakapojisikia kwamba mwili wake hauweza kuendelea tena na hapo ndipo atakapofikiria kustaafu.

No comments:

Post a Comment