BEKI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na klabu za Manchester United na Everton, Phil Neville ameamua rasmi kutundika daluga baada ya kucheza soka kwa kipindi cha miaka 18. Neville mwenye umri wa miaka 36, alitangaza April mwaka huu kwamba ataondoka Everton mwishoni mwa msimu huu ambapo sasa ana matumaini ya kufanya kazi kama kocha na pia kama mchambuzi wa mambo ya soka. Nyota huyo pia alibainisha kuwa anaweza kufanya kazi kama mchambuzi wa soka wa BBc katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil mwaka 2014. Mbali na kazi hiyo Neville pia amekuwa akifanya kazi kama mmoja wa makocha kwenye timu ya taifa ya Uingereza kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 ambao walienguliwa katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini Israel.
No comments:
Post a Comment