BEKI wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Gerard Pique amesema meneja wa zamani wa Real Madrid Jose Mourinho alikuwa akitaka kuhamisha ushindani wa timu hizo mbili uwanjani kwenda kwenye vyombo vya habari. Mourinho ambaye ameondoka Madrid baada kutoshinda taji lolote msimu uliopita na kurejea katika klabu yake ya zamani ya Chelsea, amekuwa akijulikana vyema na waandishi kwa maneno yake ya kejeli anayotoa kwa wapinzani wake. Hatahivyo, akiongea na waandishi wa habari jijini Miami, Pigue amedai kuwa tabia ya Mourinho kuhamishia ushindani wao kwa waandishi wa habari ndio chanzo kikubwa cha kukosa mafanikio Madrid. Pigue amesema timu hizo mbili zina ushindani mkubwa katika soka lakini hilo sio tatizo kwasababu inajulikana ila Mourinho alitaka kuhamisha ushindani huo kwenye vyombo vya habari kitu ambacho ni kigeni kwa Hispania ndio maana alishindwa kufanikiwa.
No comments:
Post a Comment