KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, Laurent Blanc amekanusha tetesi zinazomhusisha na kwenda kuzinoa klabu za AS Roma, Paris Saint Germain au Real Sociedad msimu ujao. Blanc ambaye ni raia wa Ufaransa amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kwenda kuinoa Roma wakati Sociedad nao waliaminika kufanya naye mazungumzo kabla ya kutangazwa Jagoba Arrasate kuchukua mikoba ya Philippe Montanier aliyeondoka. Lakini kocha huyo alijitokeza na kuthibitisha kuwa anatafuta timu ya kufundisha lakini akakanusha kwamba ameshafanya mazungumzo na klabu yoyote kati ya hizo zilitajwa. Blanc alichukua mikoba ya kuinoa Ufaransa baada ya kupata mafanikio katika klabu ya Bordeaux lakini alijiuzulu kufuatia kutolewa kwa Ufaransa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya 2012 mbele ya mabingwa wa michuano hiyo Hispania.
No comments:
Post a Comment