Friday, June 7, 2013

BOLT KUKABIDHI ZAWADI KWA MSHINDI WA FRENCH OPEN WANAUME.

SHIRIKISHO la Tenisi nchini Ufaransa limetangza kuwa mshindi wa michuano ya wazi ya Ufaransa kwa uonde wa wanaume atakabidhiwa zawadi na mkimbiaji nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt. Bolt bingwa mara sita wa michuano ya Olimpiki ambaye jana alishindwa kutamba katika mashindano ya Diamond League yaliyofanyika jijini Rome baada ya kushindwa na Justin Gatlin wa Marekani, atakuwa mwanariadha wa kwanza kupata heshima hiyo kwenye michuano mikubwa ya tenisi. Nusu fainali kwa upande wanaume inatarajiwa kufanyika leo ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo Rafael Nadal anatarajia kuchuana na Novak Djokovic ukifuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Jo-Wilfried Tsonga dhidi ya David Ferrer. Kwa upande wa wanawake ambapo fainali itafanyika Jumamosi kati ya Serena Williams na maria Sharapova, tuzo yao itakabidhiwa na bingwa mara tatu wa zamani wa michuano hiyo ambaye pia amewahi kuongoza katika orodha za ubora kwa wanawake Arantxa Sanchez Vicario wa Hispania.

No comments:

Post a Comment