KLABU ya Manchester City imetangaza kumsajili kiungo wa kimataifa wa Brazil Fernadinho kutoka klabu ya Shakhtar Donetski ya Ukraine. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa katika rada za City kwa karibu msimu mzima na anajulikana nchini Uingereza kwa kuifungia klabu yake bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi msimu uliopita. City ambao mpaka sasa hawajapa mbadala wa kocha Roberto Mancini aliyeondoka, hawakutoa taarifa zozote za kiasi cha fedha walizomnunulia mchezaji huyo lakini kumekuwa na tetesi katika vyombo vya habari nchini Uingereza kuwa amewagharimu kiasi cha paundi milioni 30. Akihojiwa Fernadinho amesema kuwa hayo ni mabadiliko, changamoto na nafasi aliyokuwa akiisubiria kwa kipindi kirefu na kuichezea City ni kama ndoto zake zimekuwa kweli.
No comments:
Post a Comment