Friday, June 7, 2013

BOLT AGARAGAZWA NA GATLIN KATIKA MBIO ZA DIAMOND LEAGUE ZA ROME.

MWANARIADHA wa mbio fupi kutoka Marekani, Justin Gatlin hatimaye amefanikiwa kumshinda bingwa wa michuano ya olimpiki, Usain Bolt wa Jamaica katika mashindano ya Diamond League yaliyofanyika jijini Rome, Italia. Bolt mwenye umri wa miaka 26 alianza kwa haraka wakati wa kuanza mbio za mita 100 lakini Gatlin alifanikiwa kuongeza nguvu na kumaliza akiwa wa kwanza kwa kutumia sekunde 9.94 wakati Bolt alishika nafasi ya pili kwa kutumia sekunde 9.95. Akihojiwa mara yam bio hizo Bolt amesema anahitaji miezi miwili ya kujiandaa kabla ya mashindano ya dunia hivyo hana wasiwasi kwasasa. Hata hivyo kwasasa Gatlin bingwa wa michuano ya olimpiki mwaka 2004 ambaye alifungiwa miaka mine kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu, anaonekana yuko katika kiwango kizuri msimu huu kwa kushinda mashindano yote aliyoshiriki.

No comments:

Post a Comment