WANADADA nyota katika tenisi Serena Williams wa Marekani na Maria Sharapova wa Urusi wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali na kutinga fainali. Williams ambaye anaongoza katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake alifanikiwa kutinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza toka 2002 aliposhinda taji la michuano hiyo kwa kumgaragaza bila ya huruma Sara Errani wa Italia kwa 6-0 6-1. Wakati Sharapova ambaye anashika namba mbili katika orodha hizo yeye alitinga hatua hiyo baada ya kumburuza Victoria Azarenka wa Belarus kwa 6-1 2-6 6-4. Wawili wanatarajia kukutana katika mchezo wa fainali utakaofanyika kesho.
No comments:
Post a Comment