TANZANIA imeendelea kutakata katika msimamo wa viwango vya ubora duniani ambavyo hutolewa na Shirikisho la Soka Dunia FIFA baada ya kupanda kwa nafasi saba mpaka kufikia nafasi ya 109. Kwa maana hiyo Tanzania sasa imezipita nchi zote za Afrika Mashariki katika viwango hivyo kasoro Uganda pekee ambao wao wako katika nafasi ya 93 baada ya kuporomoka kwa nafasi mbili mwezi huu. Kwa upande wa tano bora kwa upande wa Afrika Ivory Coast wameendelea kuongoa kwa kushinda nafasi ya 13 duniani wakifuatiwa na Ghana ambao wako katika nafasi ya 22 na nafasi ya tatu inashikiliwa na Mali ambao wao wako katika nafasi ya 23. Wengine ni Algeria waliopo katika nafasi ya 35 kwa upande wa dunia huku tano bora kwa upande wa Afrika ikifungwa na Tunisia walioko katika nafasi ya 42. Kwa upande wa orodha ya tano ya dunia Hispania waliopo katika nafasi ya kwanza, Ujerumani, Argentina na Croatia wameendelea kubakia katika nafasi zao walizokuwepo mwezi uliopita wakati kwenye nafasi ya tano kuna ingizo jipya la Uholanzi ambao wamekwea kwa nafasi nne mwezi huu.
No comments:
Post a Comment