Thursday, June 13, 2013
BRAZIL ITAKUWA TAYARI KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA.
SIKU mbili kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Shirikisho na mwaka mmoja kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA Jerome Velcke ameondoa wasiwasi kuwa Brazil haitakuwa tayari kwa michuano hiyo mikubwa. Valcke amesema miezi 12 ni muda wa kutosha wa kumalizia matengenezo katika viwanja vya ndege pamoja na viwanja 12 ambavyo vitakuwa mwenyeji wa michuano hiyo. Waziri wa Michezo wan chi hiyo, Aldo Robelo amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa viwanja vyote vitakuwa vimekamilika mpaka ifikapo muda wa mwisho ambao ni Desemba mwaka huu. Valcke aliendelea kudai kuwa kwasasa hakuna mpango mwingine tofauti na huo wa kukamilisha viwanja hivyo 12 kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa kabisa duniani. Viwanja sita kati ya 12 ndivyo ambavyo viko tayati kwa asilimia kubwa na ndivyo vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya wiki mbili ya Kombe la Shirikisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment