Thursday, June 13, 2013

HABARI ZA MIMI KUONDOKA BARCELONA NI UPUUZI - FABREGAS.

KIUNGO nyota wa klabu ya Barcelona, Csec Fabregas amekanusha tuhuma kwamba anataka kurejea nchini Uingereza baada ya kukosa namba ya kudumu katika klabu hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barcelona mwaka 2011 lakini Manchester United na klabu yake ya zamani ya Arsenal wanaaminika kutaka kumchukua mchezaji huyo kutoka Camp Nou. Fabregas amesema siku zote amekuwa na furaha Barcelona na yoyote anayesema kwamba anataka kuondoka hamjui na hajawahi kuzungumza nae.
Kiungo huyo ametokea katika shule ya vipaji ya Barcelona akiwa na miaka 10 mpaka 16 alisajiliwa na Arsenal, na ameichezea klabu hiyo mechi 303 kwa kipindi cha miaka nane na kufanikiwa kufunga mabao 57.

No comments:

Post a Comment