Monday, June 17, 2013

ETHIOPIA, TOGO, GUINEA YA IKWETA HATARINI KUKATWA ALAMA BAADA YA KUCHEZESHA WACHEZAJI WASIOSTAHILI KATIKA MECHI ZAO ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA, limesema linafazifanyia uchunguzi nchi za Ethiopia, Togo na Guinea ya Ikweta baada ya kutuhumiwa kutumia wachezaji ambao hawakustahili katika mechi zao za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia. Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa Ethiopia ambao Jumapili waliibamiza Afrika Kusini kwa mabao 2-1 na kumaliza wakiwa kileleni mwa kundi A, wanatuhumiwa kuchezesha mchezaji asiyestahili katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya Botswana uliochezwa Juni 8 mwaka huu ambao pia walishinda kwa mabao 2-1. Kama Ethiopia wakinyang’anywa alama tatu kwa kukutwa na hatia katika kosa hilo, inamaanisha Afrika Kusini bado watakakuwa na nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano kwa ajili ya kutafuta timu tano zitakazowakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo mwakani nchini Brazil. Togo nao watachunguzwa kuhusu mchezaji waliyemchezesha katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Cameroon katika kundi I mchezo ambao ulichezwa Juni 9 wakati Guinea ya Ikweta nao watachunguzwa kwa tuhuma kama hizo kwenye mchezo wao dhdi ya Cape Verde ambao walishinda mabao 4-3 Machi mwaka huu. Cemeroon watakaa kileleni mwa msimamo wa kundi lao kwa tofauti ya alama moja dhidi Libya kama wakizawadiwa ushindi katika mechi dhidi ya Togo wakati Cape Verde wao watapaa mpaka nafasi ya pili wakipishana alama mbili na vinara wa kundi B Tunisia.

No comments:

Post a Comment