Monday, June 17, 2013

MAANDAMANO YAENDELEA BRAZIL.

MICHUANO ya Kombe la Shirikisho imeendelea huku ikigubikwa na taarifa za maandamano ambayo yamepelekea baadhi ya watu kuumia wakati polisi wakijaribu kutumia risasi za mpira pamoja na mabomu ya machozi kuwatawanya. Taarifa zinadai kuwa maandamano hayo yalifikia siku ya pili toka kufunguliwa kwa michuano hiyo karibu na Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ambapo Mezico ilichabangwa mabao 2-1 na Italia. Watu kadhaa wamekamatwa wakati kuna taarifa za majeruhi baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanja waandamanaji hao ambao wanapinga gharama zilizotumiwa na serikali kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia mwakani. Waandamanaji hao wanadahani kuwa kulikuwa hakuna umuhimu wa serikali kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kujenga na kukarabati viwanja badala yake fedha hizo zingepelekwa kwenda kukuza elimu na kununua vifaa vya hospitali. Katika taarifa yake serikali ya nchi hiyo imedai kuendelea kuimarisha usalama wakati wote wa mashindano hayo ya wiki mbili na kuwahakikishia mashabiki wanaohudhuria mechi hizo usalama wa kutosha.

No comments:

Post a Comment