Thursday, June 6, 2013

ETO'O ATEULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA URUSI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa msimu wa 2012-2013. Eto’o ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne, alikabidhiwa tuzo hiyo baada ya kuisadia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wan chi hiyo. Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Eto’o ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo amedai kufurahishwa na hatua hiyo na kuwashukuru mashabiki wa soka nchini humo pamoja na waandishi wa habari kwa kuwa nyuma yake wakati wote. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 atakosa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 wa timu ya taifa ya nchi yake dhidi ya Togo utakaochezwa Juni 9 mwaka huu kutokana na majeraha yanayomsumbua.

No comments:

Post a Comment