Thursday, June 6, 2013

NIMEM-MISS DROGBA - TOURE.

KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye pia ni mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, yaya Toure amedai kuwa angependa kumuona mshambuliaji nyota wa nchi hiyo Didier Drogba katika kikosi kitakachopambana na Gambia Jumamosi. Drogba ambaye yuko likizo nchini humo alitembelea mazoezi ya timu ya taifa ya nchi hiyo waliyokuwa wakifanya katika uwanja wa Houphouet Boigny na kuwasalimia wachezaji wenzake. Toure amesema hakufurahishwa kwa Drogba kukosekana katika kikosi hicho kwasababu nyota huyo ni silaha kwa mabeki wa timu yoyote wanayokutana nayo. Kiungo huyo wa Manchester City pia alitupilia mbali tetesi kuwa yeye na Drogba hawako katika mahusiano mazuri na kudai kuwa anamheshimu nyota huyo na anamchukulia kama kaka, rafiki na mshauri wake. Kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi alimuacha Drogba katika kikosi chake na kudai kuwa anaweza kurejea tena Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment