BASI lililokuwa limepakia viongozi na wachezaji wa klabu ya E.S Bafing inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ivory Coast limeshambuliwa jana usiku wakati wakisafiri kwenda mkoa wa magharibi wan chi hiyo kwa ajili ya mchezo wa ligi hiyo. Watu waliovamia basi hilo ambao wanadhaniwa kuwa majambazi walianza kulishambulia basi hilo kwa risasi wakati dereva alipokataa amri ya kusimama na kuua mchezaji mmoja na kujeruhi wengine 23 waliokuwemo kwenye basi hilo. Kwa mujibu wa taarifa za polisi mara baada ya basi hilo kusimama watu hao wenye bunduki walivamia ndani na kupora vitu mbalimbali vya thamani vya abiria. Majambazi hayo yanahisiwa na watu wa usalama kuwa wanatoka nchi ya jirani ya Liberia ambapo huvuka mpaka kufanya uhalifu wao na kasha kurejea nchini mwao.
No comments:
Post a Comment