Saturday, June 1, 2013

FIFA YACHAGUA MWANAMKE WA KWANZA KATIKA KAMATI YAKE YA UTENDAJI.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Burundi, Lydia Nsekera amechaguliwa na kuwa mwanamke wa kwanza katika Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA katika miaka 109 ya historia ya shirikisho hilo. Nsekera mwenye umri wa miaka 46 atakuwa mjumbe ndani ya kamati hiyo kwa kipindi cha miaka minne baada ya kushinda uchaguzi wa mkutano mkuu wa FIFA uliofanyika nchini Mauritius. Mwanamama huyo alijikusanyia kura 95 kati ya kura 203 zilizopigwa akiwagaragaza Moya Dodd wa Australia na Sonia Bien-Aime aliyekuwa akiiwakilisha Uturuki na Visiwa vya Caicos. Nsekera amekuwa rais wa BFF kuanzia mwaka 2004 na pia alikuwa mjumbe wa kamati ya maandalizi ya FIFA katika michuano ya soka ya Olimpiki mwaka 2008 na 2012.
Akihojiwa mara baada ya kuchaguliwa Nsekera amesema kuchaguliwa kwake huko kutahamasisha wanawake wengi kujiamini kwamba wanaweza.

No comments:

Post a Comment