Saturday, June 1, 2013
WAZIRI APIGILIA MSUMARI WA MWISHO KUHUSU "VUVUZELA" ZA BRAZIL.
WAZIRI wa Sheria wa Brazil, Jose Eduardo Cardozo amesema vifaa vya plastini aina ya caxirola ambavyo mashabiki wa soka wa nchi hiyo hutumia kushangilia timu zao havitaruhusiwa katika viwanja wakati wa michuano ya Kombe la Shirikisho baadae mwezi huu na Kombe la Dunia mwakani kwasababu za kiusalama. Cardozo amesema sekretarieti inayosimamia matukio muhimu imeamua kuwa kwasababu za usalama wa watu wengi, itakuwa si vyema kuuhusu vifaa hivyo ndani ya viwanja. Waziri huyo aliendelea kusema kuwa adhabu ya kufungia vifaa vyovyote vya muziki ikiwemo caxirola itaanza kutekelezeka katika mchezo wa kirafiki wa kirafiki wa kimataifa kati ya Brazil na Uingereza utakaofanyika katika Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro. Caxirola ni aina vifaa vya plastiki ambavyo hutoa sauti mbalimbali kama ilivyokuwa kwa vifaa vya vuvuzela ambavyo mashabiki nchini Afrika Kusini walikuwa wakivitumia katika michuano ya Kombe la Dunia 2010. Uamuzi wa kufungia vifaa unatokana na tukio la April 28 ambapo mashabiki waliohudhuria mechi kati timu ya Bahia na Vitoria kuvurumisha mamia ya caxirola uwanjani baada ya kukasirishwa na matokeo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment