KIUNGO nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Javier Mascherano ameomba radhi baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga teke daktari wakati wa mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kati ya timu ya taifa ya nchi yake na Ecuador. Kiungo huyo ambaye kucheza katika vilabu vya Liverpool na West Ham United alitolewa baada ya kumpiga teke dereva wa gari maalumu la kubebea wachezaji walioumia dakika ya 87 ya mchezo huo.
Nyota huyo ambayo alikuwa nahodha katika mchezo huo aliomba radhi kwa tukio hilo na kudai kuwa alimuonya dereva kwa kwenda kasi mpaka kutaka kumdondosha ingawa amedai alichokifanya hakikubaliki. Katika mchezo huo Argentina ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi Ecuador na kuendelea kubakia kileleni wakiwa na alama 27 wakifuatiwa na Colombia waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 26 huku Ecuador wakibakia nafasi ya tatu wakiwa na alama 22.
No comments:
Post a Comment