Wednesday, June 12, 2013
VETTEL AONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA RED BULL.
BINGWA wa dunia wa mashindano ya Langalanga, Sebastian Vettel amekubali kuongeza mkataba na timu ya Red Bull kitendo ambacho dereva huyo raia wa Ujerumani atabakia hapo mpaka mwishoni mwa mwaka 2015. Vettel alijunga na timu ya Red Bull toka mwaka 2009, na kushinda mashindano 29 kati 39 ambayo alianza mwanzo huku akifanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya dunia. Machi mwaka 2011 dereva huyo nyota alikubali mkataba wa miaka mitatu ambao ulikuwa uishe 2014 na baada ya kufikia makubaliano Vettel aliamua kuongeza mwaka mmoja zaidi katika mkataba wake. Msimu huu Vettel ameshashinda mashindano matatu yaliwemo ya Malaysia, Bahrain na Canada yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita na pia anaongoza katika msimamo wa kuwania ubingwa wa dunia. Wiki iliyopita Vettel alidai kuwa anaweza kuachana na mbi za langalanga baada ya kipindi cha miaka mitano ijayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment