Monday, June 10, 2013
MBIO ZA UBINGWA BADO ZIKO WAZI - RED BULL.
TIMU ya Red Bull imedai kuwa mbio za ubingwa wa mashindano ya Langalanga bado ziko wazi pamoja na dereva wao Sebastian Vettel kuongeza wigo wa alama mpaka kufikia 36 baada ya kushinda mashindano ya Grand Prix ya Canada. Vettel ambaye ni raia wa Ujerumani alimshinda dereva wa timu ya Ferrari, Fernando Alonso aliyeshika nafasi ya pili na kuwa dereva wa kwanza kushinda mbio hizo mara tatu kwa mwaka huu. Lakini pamoja na mafanikio hayo Ofisa Mkuu wa Red Bull, Christian Horner ametoa angalizo kuwa yoyote anaweza kuwafikia kama wakibweteka hivi sasa hivyo wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri ili waendeleze pengo lililokuwepo. Katika msimamo huo Alonso anashika nafasi ya pili mbele ya Kim Raikkonen wa Lotus ambaye amepitwa na Vettel kwa alama 44 huku Lewis Hamilton wa Marcedes akishika nafasi ya nne wakati nafasi ya tano yup dereva mwingine wa Red Bull Mark Webber.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment