Monday, June 10, 2013
SNEIJDER ASONONESHWA KUNYANG'ANYWA UNAHODHA UHOLANZI.
KIUNGO nyota wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Galatasaray, Wesley Sneijder amekiri kupata pigo kubwa baada ya kunyang’anywa kitambaa cha unahodha wa timu yake ya taifa. Kiungo huyo alipewa unahodha wa Uholanzi wakati Louis van Gaal alipochukua nafasi ya Bert van Marwijk baada ya michuano ya Ulaya 2012. Akihojiwa Sneijder amesema ni jambo lililomuumiza sana na sio sababu hakutambua hilo ila kwasababu amekua akijitoa kwa uwezo wake wote toka akabidhiwe majukumu hayo lakini inabidi akubaliane na uamuzi wa kocha. Baada ya kumvua unahodha kiungo huyo kutokana na kutofurahishwa na kiwango chake, Van Gaal alimkabidhi majukumu hayo mshambuliaji nyota wa Manchester United Robin van Persie ambaye ameisadia klabu yake kushinda taji la Ligi Kuu msimu uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment